Rasilimali

Rasilimali za ziada

Mifumo  ya malalamiko ni muhimu kwa mradi au uwezo wa programu kutoa matokeo endelevu. Karibu kila mradi au programu, na hasa zile ambazo ni zinategemea rasilimali kwa wingi, zitakuwa na athari kwa mazingira na jamii za wenyeji, walengwa, au wadau wengine. Athari zinaweza kuwa nzuri au mbaya; au mchanganyiko wa yote mawili. Zinaweza kutofautiana kwa ukubwa  na upana, na kutokana na ugumu wa mazingira ambapo shughuli nyingi zinazofadhiliwa na Mfuko wa Mabadiliko ya Tabianchi ya Kijani (GCF) zinafanyika,  pia ni kawaida kwamba mvutano au migogoro inaweza kutokea kwa jinsi mradi au programu inavyotekelezwa.

Mifumo ya malalamiko ina jukumu muhimu katika kutoa njia zinazoaminika ili malalamiko yafikishwe mbele na matatizo kutatuliwa kabla ya kuongezeka kwa kiwango au ukali. Mara nyingi hutoa viashiria kwa mradi au watekelezaji wa programu ambapo maboresho au mabadiliko yanaweza kufanywa. Kwa hivyo, ni sehemu muhimu za mahusiano ya jamii na mikakati ya usimamizi wa hatari. Haishangazi basi kwamba pia inahitajika chini ya sera za Mfuko wa Mabadiliko ya Tabianchi ya Kijani (GCF), na kwamba Mfumo Huru wa Kupokea na Kurekebisha Malalamiko (IRM) una mamlaka ya kusaidia kuongeza uwezo wa taasisi  au mashirika yanayofikiwa moja kwa moja katika suala hili.

Kama hatua ya kuanzia, Mfumo Huru wa Kupokea na Kurekebisha Malalamiko (IRM) umekusanya rasilimali na vifaa mbalimbali ili kutoa mwongozo wa jumla na kumbukumbu kwa wale wanaotafuta kutekeleza Mfumo wa malalamiko.