Rejesta ya kesi

Wasilisha lalamiko

Wasilisha malalamiko  kwa kutumia fomu yetu ya mtandaoni

Wasilisha lalamiko Wasilisha lalamiko kwa kutumia fomu yetu ya mtandaoni. Mtu yeyote, kikundi cha watu, au jamii ambayo imeathiriwa au inaweza kuathiriwa vibaya na mradi au programu ya Mfuko wa Mabadiliko ya Tabianchi ya Kijani (GCF),· (ikiwa ni pamoja na wale wanaonufaika kikamilifu na ufadhili wa Mfuko wa Mabadilikoya Tabianchi ya Kijani - GCF) wanaweza kuwasilisha malalamiko. Mtu au watu walioathirika wanaweza kuidhinisha serikali yao au mwakilishi wao kuwasilisha na kulifuatilia lalamiko kwa niaba yao..

Lalamiko kwa Mfumo Huru wa Kupokea na Kurekebisha Malalamiko (IRM) linaweza kuwasilishwa na:

Lalalamiko linaweza kuwasilishwa kwa Kiingereza, au kwa lugha ya mlalamikaji. Ikiwezekana, tafsiri inapaswa kutolewa kwa Kiingereza. Vinginevyo, Mfumo Huru wa Kupokea na Kurekebisha Malalamiko (IRM) utajaribu kutafsiri lalamiko hilo na kujibu kwa lugha ya mlalamikaji.

Mfumo Huru wa Kupokea na Kurekebisha Malalamiko (IRM) utatoa usiri baada ya kupokea malalamiko ikiwa utaombwa kufanya hivyo na mlalamikaji. Hii ni pamoja na majina na utambulisho wa walalamikaji na wawakilishi wowote waliochaguliwa. Ambapo ufichuzi unaweza kuhitajika kushughulikia lalamiko, IRM itashauriana na mlalamikaji kabla ya kufichua taarifa yoyote ya siri.

Hakuna mahitaji rasmi ya kuwasilisha lalamiko. Mara nyingi, lalamiko linapaswa kujumuisha :

  • Jina la mlalamikaji, anwani na taarifa ya mawasiliano;
  • Ikiwa lalamiko linawasilishwa na mwakilishi wa mlalamikaji, jina na taarifa za mawasiliano za mwakilishi, pamoja na ushahidi kwamba mwakilishi anaruhusiwa kutenda kwa niaba ya mlalamikaji;
  • Maelezo ya mradi au programu ambayo imesababisha au inaweza kusababisha athari mbaya kwa mlalamikaji;
  • Maelezo ya jinsi walalamikaji wamekuwa au wanaweza kuathiriwa vibaya na mradi au programu;
  • Ikiwa usiri unaombwa na sababu zake.

Ikiwezekana pia ni muhimu kuhusisha:

  • Maelezo  ya kina ya sera na taratibu za Mfuko wa Mabadiliko ya Tabianchi ya Kijani (GCF) na / au ulinzi wa kimazingira na kijamii ambao ulikiukwa;
  • Jitihada nyingine zilizofanywa na mlalamikaji kuleta masuala hayo kujulikana kwa mifumo mingine ya malalamiko/kurekebisha  malalamiko na kama afueni, marekebisho  au msaada mwingine ulipokelewa;
  • Taarifa nyingine ambazo mlalamikaji anahisi ni muhimu au zitasaidia, kama  vile nyaraka, ripoti za vyombo vya habari, picha, video na rekodi, ambazo zinaweza kutusaidia kushughulikia malalamiko au manung'uniko yako. 

Gharama za kuwezesha kutatua tatizo na / au kufanya ukaguzi wa kufuata  taratibu  na sera zinatolewa na Mfumo Huru wa Kupokea na Kurekebisha  Malalamiko (IRM).

Ustahiki wa malalamiko

Lalamiko Iinaweza kulalamikia masuala yanayohusiana na sera au taratibu zozote za Mfuko wa Mabadiliko (GCF), ikiwa ni pamoja na zile zinazohusiana na jamii na mazingira, wenjeji, jinsia, na utoaji wa taarifa mbali ya mambo mengine. Hata hivyo, Mfumo wa Kupokea na Kurekebisha Malalamiko (IRM) hauwezi kukubali malalamiko ikiwa:

  • Linakuhusu mradi au programu ambayo Mfuko wa Mabadilko ya Tabianchi (GCF) haushiriki moja kwa moja na / au unahusika kwa njia isiyo ya moja kwa moja;
  • Linazohusiana na idara za Mfuko wa Mabadiliko ya tabianchi sisizohusina na uendeshaji wa mazingira safi, mazuri na salama, kama vile rasilimali watu na fedha;
  • Linalohusiana na tuhuma za rushwa au masuala ya manunuzi (malalamiko haya yanashughulikiwa na Kitengo Huru cha Uadilifu (IIU) na Vitengo vingine vya Mfuko wa Mabadiliko ya Tabianchi (GCF);
  • Pale tu ambapo sera na taratibu za Mfuko wa Mabadiliko ya Tabianchi zinajitosheleza;
  • Kuhusu jambo ambalo tayari limeshughulikiwa na Mfumo Huru wa Kupokea na Kurekebisha Malalamiko (IRM), isipokuwa kama kuna habari mpya muhimu ambayo haikupatikana hapo awali; au
  • Ni mbaya, ya kipuuzi  na / au ya udanganyifu au imewasilishwa  ili kupata faida ya kiushindani.

Mchakato wa lalamiko

Mara tu baada ya lalamiko kuwasilishwa, Mfumo Huru wa Kupokea na Kurekebisha MalalamikoI (RM) utaamua ikiwa linastahiki, na unaweza kuomba habari zaidi kutoka kwa mlalamikaji kufanya uamuzi huu. Uamuzi wa ustahiki ni kwa asili yake ni wa utaratibu, na haumaanishi kuwa ni uamuzi au hukumu inayotolewa na  IRM juu ya masuala katika lalamiko au sifa zao.

Mara tu baada ya lalamiko kuonekana linastahili, Mfumo Huru wa Kupokea na Kurekebisha Malalami (IRM) utawasiliana na mlalamikaji na wengine wanaohusika kuchunguza ikiwa kesi hiyo ina sifa  za utatuzi wa tatizo kupitia michakato shirikishi, kama kubadilishana taarifa au upatanishi.

Ikiwa walalamikaji na wengine wako tayari kushiriki katika mchakato wa kutatua tatizio, Mfumo Huru wa Kupokea na Kurekebisha Malalamiko (IRM) utasaidia kubuni na kuwezesha mchakato unaolenga kufikia suluhisho la kuridhisha pande zote  zinazoshughulikia lalamiko. Ikiwa makubaliano yatafikiwa, IRM itafuatilia utekelezaji wa makubaliano kwa kushauriana na washirika.

Ikiwa hakuna nia ya kushiriki katika mchakato wa kutatua tatuzo au mchakato wa kutatua tatizo hauwezi kutatua tatizo husika kwa ufanisi, Mfumo wa Kupokea na Kurekebisha Malalamiko (IRM) utajihusisha kutathmini lalamiko. Tathmini inalenga kuamua kama kuna ushahidi wa kutosha kwamba Mfuko wa Mabadiliko ya Tabianchi (GCF) imekiuka sera na taratibu zake. Tathmini inazingatia taarifa zinazotolewa na mlalamikaji, pamoja na majibu kutoka kwa Sekretarieti ya GCF.

Ikiwa Mfumo wa Kupokea na Kurekebisha Malalamiko (IRM) utaamua ya kuwa kuna uwezekano wa ushahidi wa kutosha wa ukiukaji wa sera na tarabibu, Mfumo wa Kupokea na Kurekebisha Malalamiko (IRM) utachunguza masuala yaliyoibuliwa katika malalamiko ili kuamua ikiwa ukiukaji wowote wa sera na taratibu za Mfuko wa Mabadiliko ya Tabianchi ya Kijani (GCF) zimefanyika. IRM inaweza kufanya mahojiano, kusoma taarifa za tovuti na kusoma maandiko ili kujua ukweli halisi wa mambo.

Rasimu ya ripoti ya uchunguzi ya Mfumo wa Kupokea na Kurekebisha Malalamiko (IRM) inatumwa kwa mlalamikaji na Mfuko wa Mabadiliko ya Tabianchi ya Kijani (GCF) kwa ajili ya mrejesho. Mara baada ya kukamilika, ripoti itawasilishwa kwa bodi ya GCF, pamoja na mapendekezo yoyote, kwa ajili ya uamuzi.

Kwa haraka iwezekanavyo, Bodi ya Mfuko wa Mabadiliko ya Tabianchi ya Kijani, itaipititia ripoti na kuamua iwapo ifanye marekebisho na kutoa afuaeni kwa mlalamikaji.

Ikiwa Bodi·itaamua kufanya marekebisho, Mfuko wa Mabadiliko ya Tabianchi ya Kijani (GCF) utaamua kuandaaa mpango ili kurekebisha lalamiko. Mfumo wa Kupokea na Kurekebisha Malalamiko utafuatilia hali hiyo kuhakikisha hiyo hali imeshughulikiwa.

Wasiliano na mifumo  nyingine ya malalamiko

Malalamiko yanaweza pia kuwasilishwa kwa mifumo yakurekebisha malalamiko ya taasisi au mashirika yaliyoidhinishwa ya Mfuko wa   Mabadiliko ya Tabianchi ya Kijani. Kuna taasisi au mashirika mengine yaliyoidhinishwa   ambayo malalamiko yao yanapaswa kuwasilishwa moja kwa moja kwa Mfumo Huru wa Kupokea na Kurekebisha Malalamiko (IRM).