Kuhusu Mfumo Huru wa Kupokea na Kurekebisha Malalamiko (IRM)

Dhima

Dhima ya wa Mfumo Huru wa Kupokea na Kurekebisha Malalamiko (IRM) ni kushughulikia malalamiko kutoka kwa watu walioathirika na kutoa njia mbadala katika namna ambayo ni ya haki, yenye ufanisi na ya uwazi, na kuongeza utendaji wa Mfuko wa Mabadiliko ya Tabianchi (GCF) kutoa ufadhili wa kifedha kwa mabadiliko ya tabianchi. IRM pia inakubali maombi kutoka kwa Nchi zinazoendelea zinazohitaji kufikiriwa upya maombi ya kupata ufadhili wa fedha ambayo awali yalikataliwa na Bodi ya GCF.

Mfumo Huru wa Kupokea na Kurekebisha Malalamiko (IRM) una mamlaka ya kutoa ushauri kwa bodi ya Mfuko wa Mabadiliko ya Tabianchi ya Kijani (GCF) juu ya sera na taratibu za uendeshaji, kulingana na masomo yaliyojifunzwa kutoka katika masuala yetu . Kwa kutambua kwamba taasisi au mashirika yanayofikiwa moja kwa moja· yanaweza kuhitaji msaada wa kutengeneza· taratibu zao za mfumo wa malalamiko, IRM pia imepewa mamlaka ya kutekeleza programu kwa aina hizo za kujenga uwezo. 

Utawala

Mfumo Huru wa Kupokea na Kurekebisha Malalamiko (IRM) ni Huru kwa Sekretarieti ya GCF, na unaripoti moja kwa moja kwa Bodi ya GCF, ambayo inasimamia uwekezaji na usimamizi wa Mfuko. Awali Mamlaka ya IRM·iliundwa na Bodi ya GCF kwa kutumia Hadidu Rejea (TOR) za Mwaka 2013, na imeelezwa katika maamuzi kadhaa ya Bodi. Hadidu Rejea za IRM ziliboreshwa baada ya mfululizo wa mashauriano ya ndani na nje. Bodi ilipitisha Hadidu Rejea za IRM mwaka 2017 kutoka katika Taratibu na Miongozo ya IRM zilipitishwa za mwaka 2019.

Kazi ya Mfumo Huru wa Kupokea na Kurebisha Malalamiko (IRM) inafanywa kwa mujibu wa taratibu na miongozo yake na Hadidu Rejea zake zilizoboreshwa , ambazo zinanaelezea jinsi IRM  na vitengo vyake vinavyofanya kazi, na jinsi kesi zitakavyoshughulikiwa.

Sera za Mfuko wa Mabadiliko ya Tabianchi ya Kijanni (GCF)

Ili kutekeleza mamlaka yake, IRM inaongozwa na sera kadhaa za Mfuko wa Babadiliko ya Tabianchi ya Kijani (GCF) zinazohusiana na shughuli za kawaida za GCF na miradi na mipango yake.

Washirika

Uundwaji wa Mifumo Huru wa Uwajibikaji au mifumo  ya kutoa msaada wa kwa malalamiko (IAMs) kwa sasa inachukuliwa kuwa ni utaratibu bora zaidi unaofanywa na taasisi za kifedha za kimataifa, mashirika ya maendeleo ya kimataifa na taasia au mashirika mengine yanayofanana na hayo.

Mfumo Huru wa Kupokea na Kurekebisha Malalamiko (IRM) unafanya kazi kwa kushirikiana na mifumo mingine ya kurekebisha malalamiko na uwajibikaji, ambayo  baadhi yao inamilikiwa na taasisi au mashirika  yalivyoidhinishwa na GCF, ambayo yanaelekeza rasilimali za GCF kwa nchi zinazoendelea.

Mitandao ya Mifumo Huru ya Uwajibiakaji (IAMnet)

Mfumo Huru wa Kupokea na Kurekebisha Malalamiko (IRM) ni mwanachama wa Mtandao Huru wa Uwajibikaji (IAMnet),ambao ni mtandao wa watendaji waliojitolea kubadilishana mawazo na kusaidia taasisi kujenga uwezo· katika maeneo ya uwajibikaji na kufuata taratibu na sera kama hatua bora ya utawala wa pamoja wa shirika.