Kuhusu Mfumo Huru wa Kupokea na Kurekebisha Malalamiko (IRM)

Wajibu na kazi

Hadidu Rejea (TOR)  ya mwaka 2017 za Mfumo Huru wa Kupokea na Kurebisha Malalamiko (IRM) hutoa kazi tano za kutoa marekebisho na kuendeleza uwajibikaji katika Mfuko wa Mabadiliko ya Tabianchi ya  Kijani.

IRM inashughulikia maombi kutoka katika nchi inayoendelea ya kufikiriwa upya ya  mradi au programu yake yaliyokataliwa ufadhili  na maamuzi ya Bodi ya GCF. Baada ya ombi la kufikiriwa upya kuonekana linafaa, IRM inafanya mchakato wa taarifa na mashauriano ili kuona kama njia muafaka inayokubalika kwa ajili ya pendekezo la ufadhili inaweza kupatikana. Ikiwa hii haijafanikiwa, IRM inafanya uchunguzi ili kuamua ikiwa uamuzi wa Bodi ulitokana na kutofuata sera au taratibu za GCF , na  kwa msingi huo, inaweza kupendekeza kufikiriwa upya katika  Bodi.

IRM inashughulikia manung'uniko na malalamiko kutoka kwa watu walioathirika vibaya na miradi au mipango ya GCF. Baada ya kuthibitisha ustahiki, IRM inashirikiana na washirika husika kuchunguza chaguzi za kutatua matatizo yaliyooneshwa katika lalalamiko, kwa lengo la kupata matokeo yanayoridhisha pande zote. Ikiwa washirika katika majadiliano·hawapotayari au hawawezi kutatua masuala hayo, IRM inafanya tathmini kufuata taratibu na sera kung'amua kama uchunguzi ulifuata vigezo stahiki , na ikiwa haukufuata , itaafanya uchunguzi ili kutambua sera au taratibu zozote za GCF zinazohusiana na lalamiko ambazo hazikufuatwa na kupendekeza hatua stahiki za marekebisho. IRM inafuatilia mchakato wowote wa usuluhishi ua mapendekezo yoyote ya kufuata· sera na tarattibu yanayotokana na mchakato huo.

Kulingana na masomo yaliyojifunza kutoka katika kesi zake na kazi au mazoea mazuri ya kimataifa, Mfumo Huru wa Kupokea na Kurekebisha Malalamiko (IRM) hutoa ushauri wa kimfumo kwa Mfuko wa Mabadiliko ya Tabianchi ya Kijani (GCF) juu ya sera na taratibu kwa jicho la kuboresha utandaji na matokeo ya Mfuko wa Mabadiliko ya Tabianchi ya Kijani (CGF). Lengo la jukumu hili ni kutambua masomo yaliyofifunzwa na kutoa mrejesho kwa GCF na taasisi au mashirika mengine ili kuboresha utendaji na matokeo ya shughuli za Mfuko wa Mabadiliko ya Tabianchi ya Kijani (GCF)

Katika kutimiza  wajibu huu, IRM inalenga kutoa ushauri juu ya sera na taratibu, badala ya ushauri maalum wa mradi. Ushauri unaotolewa na IRM unaweza kuchukua sura tofauti kama vile:

  • Mawasiliano ya moja kwa moja kwa Sekretarieti ya GCF au Bodi ya GCF na Kamati ya Maadili na Ukaguzi
  • Warsha na matukio mengine ya kujifunzia
  • Shughuli za Nje ya sehemu za kazi 
  • Uzalishaji wa vifaa, miongozo au machapisho

Mfumo wa Kupokea na Kurekebisha Malalamiko (IRM) unafanyakazi na Taasisi na Mashirika yanayofikiwa  moja kwa moja ili kuwasaidia kujenga uwezo unaohusiana na mifumo na taratibu za malalamiko. Utajihusisha kujenga uhusiano na taasisi au mashirika ili kuelewa mahitaji yao kwa ubora na kutambua njia bora zaidi za kuwaimarisha. Shughuli za kujenga uwezo za IRM zinaweza kuchukua sura ya: 1) Warsha na mafunzo; 2) vipindi vya kutoa habari; 3) usambazaji wa mafunzo yaliyojifunzwa na rasilimali nyingine juu ya mifumo wa malalamiko na kuyarekebisha.

IRM imeunda kozi ya mafunzo ya mtandaoni juu ya dhana muhimu zinazohusiana na Mifumo ya Kurekebisha Malalamiko, ambayo inapatikana kwenye  "jukwaa la kujifunza la mtandaoni la Mfuko wa Mabadiliko ya Tabianchi ya Kijani (GCF)". Kimsingi ikiwa imeundwa kwa ajili ya kuimarisha Mifumo ya Kurekebisha Malalamiko (GRMs) ya taasisi na mashirika ya Mfuko wa Mabadiliko ya Tabianchi ya Kijani (GCF), kozi hii ina manufaa sawa kwa watu binafsi na taasisi zinazopenda kujifunza namna ya kuunda na kutekeleza Mfumo wa Kurekebisha Malalamiko (GRM) wenye ufanisi.

Taasisis au Mashirikana yanayofikiwa  moja kwa moja na yaliyo na nia ya jukumu la kujenga uwezo wa Mfumo Huru wa Kupokea na Kurekebisha Mlalamiko yanapaswa kuwasiliana nasi moja kwa moja.

Mfumo wa Kupokea na Kurekebisha Malalamiko (IRM) unataka kuongeza ufahamu juu ya kazi yake, na kugawana mafunzo yanayotokana na uzoefu wake na wadau wengine pamoja na umma kwa ujumla. Unalenga kuongeza ufahamu wa wajibu wake na kazi zake kati ya walalamikaji na waombaji, mashirika ya kiraia na umma kwa ujumla.

Jinsi tunavyofanya kazi

Wakati wa kuzishughulika kesi, Mfumo wa Kupokea na Kurekebisha Malalamiko (IRM) una michakato kadhaa ya kushughulikia masuala yaliyoibuliwa katika maombi au malalamiko.

Kutatua tatizo

Mfumo wa Kupokea na Kurekebisha Malalamiko (IRM) unafanya kazi na wadau kwa njia mtambuka na shirikishi ili kutatua masuala na kushughulikia malalamiko. Utatuzi wa tatizo unaweza kuwa wa ushirikishwaji wa habari na mashauriano, uwezeshaji, upatanishi, kutafuta ukweli kwa pamoja, na nyenzo zingine. Mazoea ya Mfumo wa Kupokea na Kurekebisha Malalamiko (IRM) yanaongozwa na kanuni mbadala za utatuzi wa migogoro (ADR).

Lengo la mchakato wa kutatua tatizo ni kushughulikia masuala maalum ambayo yamepelekea kuibuka ombi au lalamiko, na kusaidia kutambua na kukubaliana na ufumbuzi unaokidhi maslahi ya pande zote. Kwa kawaida unahusisha ufafanuzi wa dukuduku husika, kuelewa mahitaji na maslahi ya wadau, kusaidia washirika kutambua ufumbuzi, na kuwasaidia kufikia makubaliano juu ya masharti ya ufumbuzi huu.

Kuna kanuni kadhaa zinazoimarisha mchakato wa kutatua tatizo la Mfumo wa Kupokea na Kurekebisha Malalamiko (IRM).

  • Hiari: - Utatuzi wa tatizo unawezekana pale tu ambapo washirika wapo tayari kushiriki na kufanya kazi pamoja. Hakuna mshirika anayelazimishwa kushiriki au kukubaliana na njia ya utatatuzi wa suluhisho maalumu. Washiriki katika mgogoro wana haki ya kujiondoa kutoka katika mchakato wa kutatua tatizo ikiwa haukidhi mahitaji yao.
  • Unawezeshwa: - Utatuzi wa tatizo kwa kawaida unaofanywa na mtu au chombo kisichopendela upande wowote, wanaweza kuwa ni wafanyakazi wa IRM au mshauri wa kujitegemea, ambao jukumu lao ni kukutanisha na kuwezesha uhusishwaji wa pande zote katika utatuzi wa mgogoro. Mshirika asiyependelea upande wowote hafanyi maamuzi juu ya suala linalojadiliwa, bali hujikita kusimamia mchakato. Wanalenga kutopendela upande wowote au kutojiusisha kwa undani na pande zote, na kutojihusiaha na kufanya maamuzi juu ya jambo lenye dukuduku na huwa wanakuwa na ujuzi stahiki wa kitamaduni na wa lugha ili kufanya kazi kwa ufanisi na wadau wa jamii husika.
  • Ni shirikishi na Huzingatia maslahi ya washirika - Washirika katika mchakato wa kutatua mgogoro ni waamuzi wakuu na waendeshaji wa mchakato huo. Mchakato - huhusisha sheria, ajenda, masuala, ufumbuzi, makubaliano na utekelezaji - hufafanuliwa na kutekelezwa kwa idhini yao tu.
  • Nyumbulika - Kwa asili yake utatatuzi wa tatizo ni nyumbulika na mchakato unaweza kubadilishwa kulingana na mahitaji ya washirika. Upeo unaweza kupanuliwa au kupunguzwa, na watu au vyombo vingine wanaweza kualikwa kushiriki pale ambapo inafaa kwa masuala husiaka.
  • Ni Siri: - Utatuzi wa tatizo hufanyika katika nafasi ya usiri uaoamuliwa na washirika. Kama ilivyo sheria, kwa ujumla, taarifa iliyowekwa wazi na majadiliano huchuliwa kama sehemu ya mchakato wa kutatua tatizo na ni siri, isipokuwa pale ambapo washirika wamekubaliana kuyafichua.

Hujikita katika majadiliano na wadau wakuu katika lalamiko au ombi. Mfumo wa Kupokea na Kurekebisha Malalamiko (IRM) utashirikiana nao kuendeleza mchakato wa kutatua tatizo uliokubaliwa kwa pamoja. Hii inalenga kushughulikia masuala yaliyoibuliwa au, pale ambapo mchakato wa kutatua tatizo hauwezekani. Rejea suala la uhakiki wa kufuata taratibu na sera za Mfumo wa Kupokea na Kurekebisha Malalamiko (IRM).

Michakato ya kufuata sera na taratibu

Mfumo wa Kupokea na Kurekebisha Malalamiko (IRM) unafanya tathmini na uchunguzi huru wa miradi na programu za Mfuko wa Mabadiliko ya Tabianchi ya Kijani (GCF) na ufuataji wao wa sera na taratibu za GCF. Unaatoa mapendekezo kwa Bodi ya GCF kulingana na ukaguzi wake kwa nia ya kuhakikisha ufuataji wa taratibu na sera na ufanyaji wa marekebisho.

Lengo la mchakato wa kufuata taratibu na sera ni kuamua kama sera au taratibu zozote za Mfuko wa Mabadiliko ya Tabianchi (GCF) zimekiukwa na, ikiwa ni hivyo, hutoa mapendekezo ya namna ya kurekebisha au tiba inayopaswa kutolewa. Michakato ya kufuata taratibu na sera inalenga GCF na ufuataji wa sera na taratibu zake husika katika mradi maalum. Uchunguzi wa kufuata taratibu na sera wa Mfumo wa Kupokea na Kurekebisha Malalamiko (IRM) ni huru, lakini ni nyongeza kwa taratibu za Mfuko wa Mabadiliko ya Tabianchi ya Kijani (GCF) kwa ajili ya kuhakisha ufuataji wa taratibu na sera za mradi.

Tathmini na uchunguzi wa kufuata taratibu na sera zinaweza kuja baada ya:

  • Kama ombi la kufikiria upya ufadhili wa kifedha halijashughulikiwa kwa kutolewa taarifa na kufanyiwa majidiliano kiasi cha kuridhika kwa mwombaji;
  • Kama mlalamikaji au wadau wengine muhimu hawapo tayari kushiriki katika mchakato wa kutatua tatizo;
  • Kama mchakato wa kutatua tatizo hausababishi makubaliano au haushughulikii masuala yenye dukuduku;
  • Mfumo wa Kupokea na Kurekebisha Malalamiko (IRM) unaanzisha uchunguzi juu ya mpango wake mwenyewe, kulingana na habari za kuaminika zinazoelezea uwezekano wa ukiukwaji wa kesi pale ambapo walalamikaji hawawezi kufikia IRM moja kwa moja. 

Mapitio ya kufuata sera na taratibu  ya Mfumo Huru wa Kupokea na Kurekebisha Malalamiko (IRM) ni mchakato unaohusisha hatua mbili ambapo: 1) tathmini ya kufuata sera na taratibu inafanywa ili kuamua ikiwa kuna ushahidi wa kutosha kuonesha kwamba ukiukwaji wa sera za  GCF umefanyika, na 2) uchunguzi wa kufuata sera na taratibu unafanywa ili kuamua kama ukiukwaji wa kweli ulifanyika, na kutoa mapendekezo kwa  Bodi ya GCF juu  ya namna huu uvunjaji wa sera na taratu , kama ipo, unaweza kurekebishwa.

Katika kufanya uchunguzi wake wa kufuata taratibu na sera, kwa kawaida IRM  huajiri wataalam bobezi huru kufanya uchunguzi wa suala mahsusi, au huajiri wataalam bobezi wengine pale wanapohitajika kusaidia IRM katika uchunguzi wake.

Ikiwa Mfuko wa Mabadiliko ya Tabianchi ya Kijani (GCF) utaonekana ya kuwa unafuata sera na taratibu zake, Mfumo Huru wa Kupokea Kurekebisha  Marekebisho (IRM) utanawasilisha ripoti yake kwa Bodi ya GCF na hautachukua hatua zaidi. Katika suala·la maombi ya ufafadhili, ambayo GCF imeonekana hutokuyakubali, IRM hupendekeza ya kwamba, Bodi ifikirie tena pendekezo la ufadhili ambalo lilikataliwa. Katika suala la·malalamiko, ambapo GCF imeonekana kuyakataa, na Bodi·imeruhusu marekebisho, IRM·hufuatilia utekelezaji wa marekebisho kama hayo na / au majibu ya Sekretarieti ya GCF, ikiwa ni pamoja na mipango yoyote ya kurekebisha ambayo imewekwa.

Ufuatiliaji

Mfumo Huru wa Kupokea na Kurekebisha Malalamiko  (IRM) una mamlaka ya kufuatilia makubaliano ya washirika husika katika mchakato wa usuluhishi au utekelezaji wa marekebisho yoyote yatakayojitokeza au majibu ya Sekretarieti ya GCF, ikiwa ni pamoja na mipango yoyote ya kurekebisha.