Rejesta ya kesi

Wasilisha ombi la kufikiriwa upya

Wasilisha ombi la kufikiriwa upya kwenye fomu yetu ya mtandaoni

Wasilisha ombi la kufikiriwa upya:· Wasilisha ombi la kufikiriwa upya kwa kutumia fomu yetu ya mtandaoni. Nchi inayoendelea inaweza kuwasilisha ombi iwapo moja kati ya miradi yake maalumu· au mipango iliyopendekezwa kwa Mfuko wa Mabadiliko ya Tabianchinya Kijani (GCF) imekataliwa na bodi ya GCF kwa sababu nyingine mbali na ukosefu wa rasilimali za GCF. Ombi linaweza kuwasilishwa na Mamlaka Iliyoteuliwa Kitaifa Kushughulikia Masuala ya GCF kwa Muda Mrefu (NDA) au mamlaka nyingine· au Mamlaka nyingine yoyote au wakala wa nchi. Nchi inayoomba lazima iamini kwamba kukataliwa ufadhili wa fedha kulitokana na kutofuata "Sera au taratibu za GCF"..

Ombi la kufikiriwa upya ufadhilli wa  fedha linapaswa kuwasilishwa ndani ya siku 60 kutoka tarehe ambayo kukataaliwa ufadhili wa fedha kulitaarifiwa na Sekretarieti kwa Mamlaka Iliyoteuliwa Kitaifa Kufanya Kazi za GCF (NDA).

Ombi linapaswa kuelezea mradi au programu ambayo ilikataliwa fedha na bodi ya Mfuko wa Mabadiliko ya Tabianchi ya Kijani (GCF), na lihusishe maelezo ya hali iyosababisha kutofuata taratibu na sera na ni kwa jinsi gani hali hii zilisababisha kukataliwa ufadhili wa fedha. Ombi linapaswa pia kuthibitisha kwamba taasisi au shirika liliyoidhinishwa na ambalo  liliwasilisha pendekezo bado lina nia ya kutekeleza mradi au programu, iwapo litapewa ufadhili wa fedha hapo baadaye na GCF.

Taarifa yoyote ya kweli katika ombi inapaswa kuambatana na nyaraka saidizi na ushahidi mwingine unaofaa. Maombi yanaweza kuwasilishwa kwa Kiingereza au kwa lugha nyingine yoyote ya Umoja wa Mataifa, zikiambatana na tafsiri za Kiingereza.

Ombi linaweza kuwasilishwa kwa barua pepe, mjumbe au kutuma barua pepe kwa Mfumo Huru wa Kupokea na Kurekebisha Malalamiko (IRM), au kwa kujaza fomu kwenye tovuti.

Mchakato wa kufikiria  ombi  upya

Mara tu ombi linapopokelewa, Mfumo wa Kupokea na Kurekebisha Malalamiko (IRM)  huamua ikiwa ombi linastahki, na kumjulisha mwombaji na Sekretarieti ya GCF.

Pale ombi litaonekana linastahiki, Mfumo wa Kupokea na Kurekebisha Malalamiko (IRM) utafanya majadiliano na mwombaji na  wafanyakazi wa Mfuko wa Mabadiliko ya Tabianchi ya Kijani(GCF). Inaweza pia kushauriana na wadau wengine kuchunguza kama kupitia habari na mashauriano hali hiyo inaweza kurekebishwa au kama mwombaji angependa IRM kuchunguza masuala husika.

Ikiwa mwombaji ameridhika baada ya mchakato wa kupata habari na mashauriano, Mfumo Huru wa Kupokea na Kurekebish Malalamiko (IRM) utafunga kesi hiyo. vinginevyo, IRM itaanza uchunguzi.

Ripoti ya uchunguzi itawasilishwa kwa kwa Bodi ya Mfuko wa Mabadiliko ya Tabianchi ya Kijani (GCF), kupendekeza kama Bodi inapaswa kufikiria upya uamuzi wake wa fedha na sababu za mapendekezo.

Bodi ya Mfuko wa Mabadiliko ya Tabianchi ya Kijani (GCF) itawasilisha maamuzi yake kwa Mfumo wa Kuokea na kurekebisha Malalamiko (IRM), ambao utamtaarifu mwombaji.