Rasilimali nyingine
Rasilimali za ziada
Mifumo ya malalamiko ni muhimu kwa mradi au uwezo wa programu kutoa matokeo endelevu. Karibu kila mradi au programu, na hasa zile ambazo ni zinategemea rasilimali kwa wingi, zitakuwa na athari kwa mazingira na jamii za wenyeji, walengwa, au wadau wengine. Athari zinaweza kuwa nzuri au mbaya; au mchanganyiko wa yote mawili. Zinaweza kutofautiana kwa ukubwa na upana, na kutokana na ugumu wa mazingira ambapo shughuli nyingi zinazofadhiliwa na Mfuko wa Mabadiliko ya Tabianchi ya Kijani (GCF) zinafanyika, pia ni kawaida kwamba mvutano au migogoro inaweza kutokea kwa jinsi mradi au programu inavyotekelezwa.
Mifumo ya malalamiko ina jukumu muhimu katika kutoa njia zinazoaminika ili malalamiko yafikishwe mbele na matatizo kutatuliwa kabla ya kuongezeka kwa kiwango au ukali. Mara nyingi hutoa viashiria kwa mradi au watekelezaji wa programu ambapo maboresho au mabadiliko yanaweza kufanywa. Kwa hivyo, ni sehemu muhimu za mahusiano ya jamii na mikakati ya usimamizi wa hatari. Haishangazi basi kwamba pia inahitajika chini ya sera za Mfuko wa Mabadiliko ya Tabianchi ya Kijani (GCF), na kwamba Mfumo Huru wa Kupokea na Kurekebisha Malalamiko (IRM) una mamlaka ya kusaidia kuongeza uwezo wa taasisi au mashirika yanayofikiwa moja kwa moja katika suala hili.
Kama hatua ya kuanzia, Mfumo Huru wa Kupokea na Kurekebisha Malalamiko (IRM) umekusanya rasilimali na vifaa mbalimbali ili kutoa mwongozo wa jumla na kumbukumbu kwa wale wanaotafuta kutekeleza Mfumo wa malalamiko.
- Ripoti ya Kujitambua ya Mfumo Huru wa Kupokea Kurekebisha Malalamiko (IRM)
- Zana ya Mfumo wa Malalamiko za Mtaalamu Aliyeteuliwa Kusimamia Ufuataji wa Sera na Taratibu (CAO)
- Mwongozo wa Programu ya Pamoja ya Kituo cha Pamoja cha Hewa Ukaa ya Misitu (FCPF) /Chombo Kikuu cha Ushirikiano wa Ufahamu na Ushauri cha Umoja wa Mataifa juu ya Misitu na Tabianchi kwa ajili ya Kupungaza Hewa Ukaa katika Misitu na Kuwezesha Uhifadhi wa Hewa Ukaa (UN-REDD), Angalizo kwa Taasisi ya Kupunuza Hewa Ukaa inayotokana na Kukata Miti na Upungufu wa Misitu Katika Nchi Zinzaoendelea (REDD) + Nchi: Kuanzisha na Kuimarisha Mifumo ya Malalamiko.
- Sanduku la Vifaa vya Mfumo wa Malalamiko la Jamii ya Chama cha Kimataifa cha Kuhifadhi Mazingira cha Sekta ya Petroli (IPIECA's)
- Wajibu wa Kampuni wa Kuheshimu Haki za Binadamu: Mwongozo Unaotafsirika
- Miongozo wa Kanuni za Umoja wa Mataifa kuhusu biashara na haki za binadamu
- Mazoea ya Kurekebisha Malalamiko ya Benki ya Dunia
- Angalizo la Mazoea Mazuri ya Shirika la Fedha la Kimataifa (IFC): Kushughulikia Malalamiko kutoka kutoka katika Jamii Zilizoathiriwa na Mradi
- Ripoti ya IIED juu ya Usuluhishi na mgogoro unaohusiana na maendeleo
- Mradi wa Uwajibikaji na Tiba wa OHCHR
- Mwongozo wa OHCHR juu ya Kukidhi Vigezo vya Ufanisi wa UNGPs
- The Independent Accountability Mechanisms Network: Criteria for participation and principles for cooperation