C0003 Morocco

FP043: Mradi wa Kuhifadhi Maji wa Saïss

C0003 Morocco

  • Aina yalalamiko
  • Tarehe iliyopokelewa 16 Februari 2020
  • Matokeoya kesi Makubalino ya utatuzi wa tatizo yamewekwa

Mnamo Februari 16, 2020, IRM ilipokea malalamiko ambayo yaliwasilishwa kupitia Mfumo wake wa Usimamizi wa Kesi mtandaoni (CMS). Mlalamikaji alikuwa ametoa ombi la usiri, na IRM ilitoa usiri kwa mujibu wa Taratibu na Miongozo yake (PGs). Malalamiko yanayohusiana na GCF mradi uliofadhiliwa FP043, Mradi wa Uhifadhi wa Maji wa Saïss, ulioko katika Uwanda wa Saïss nchini Morocco. Malalamiko hayo yaliibua masuala yanayohusu utoshelevu wa mashauriano yaliyofanyika na ukosefu wa taarifa zinazotolewa kwa mlalamikaji na wengine walioathirika na Mradi huo. Malalamiko hayo pia yaliibua wasiwasi unaohusiana na ukosefu wa taarifa na mawasiliano juu ya upatikanaji wa maji na uwezo wa upatikanaji huo. Malalamiko hayo yalitangazwa kuwa yanastahili kuchakatwa zaidi na IRM tarehe 7 Aprili 2020. 

Wakati wa kufanya mashauriano yaliyofanyika katika hatua ya awamu ya awali, wahusika wa pande zote vilikubaliana kuanza kutatua matatizo mnamo tarehe 6 Juni mwaka 2020. Tangu tarehe hiyo, licha ya changamoto zinazosababishwa na Uviko-19 kwa njia ya vikwazo vya kusafiri na vikwazo vya kukutana ana kwa ana na kwenda makazini, mikutano mingi ya kimtandao ilifanyika ikihusisha pande tofauti kwa msaada wa timu ya usuluhishi ya Mfumo wa Kupokea na Kurekebisha Malalamiko (IRM). Wakati wa mikutano hiyo, mlalamikaji alifutilia mbali ombi lake la usiri. Kutokana na juhudi hizi, mlalamikaji na Wizara ya Kilimo na Uvuvi wa Baharini wa Morocco walifikia makubaliano kadhaa.  Mfuko wa Mabadiliko ya Tabianchi ya Kijani (GCF) na taasisi au mashishirika yaliyoidhiniswa, Benki ya Ulaya ya Ujenzi na Maendeleo (EBRD), katika majukumu yao kama waangalizi wa mchakato huo, wamethibitisha kupokea na kuzingatia maudhui ya makubaliano. Mlalamikaji pia aliwasiliana juu ya kuridhika kwake na matokeo ya mchakato huo na nia yake ya kusitisha malalamiko wakati huu, kwa ufahamu kamili kwamba Mfumo Huru wa Kupokea na Kurekebisha Malalamiko (IRM) hautahusika katika ufuatiliaji wa makubaliano yaliyofikiwa na pande zote.

Kwa kuzingatia ukweli huu, Mfumo Huru wa Kupokea na Kurekebisha Malalamiko (IRM) umeamua kusitisha na kufunga kesi hii.

Hali ya kesi

Fungua

Tarhe 16 Februari 2020

Uhalali / Uchunguzi wa Awali
Hatua za Awali na uchaguzi wa Mchakato
Kutatua tatizo
Imefungwa

Tarehe 26 Agosti 2021 - Makubaliano  ya kutatua tatizo yamefikiwa

Mlalamikaji

Siri

Hali halisi ya madhara iliyotolewa

Mashauriano
Upatikanaji wa maji
Ufichuaji wa taarifa

Sera za Mfuko wa Mabadiliko ya Tabianchi (GCF) zilizoibuliwa

Viwango vya kimazingira na kijamii
Sera ya kimazingira na kijamii

Uwekaji kumbukumbu

Kichwa cha habari Matoleo
Uamuzi  wa Ustahiki
Kiingereza| العربية
Refusho la kikomo cha muda kwa uchapishaji wa ripoti ya hatua za awali.
Kiingereza| العربية
Ripoti ya hatua za awali
Kiingereza| العربية
Refusho la kikomo cha muda kwa ajili ya kutatua tatizo
Kiingereza| العربية
 Kumbukumbu za utatuzi wa tatizo 
Kiingereza| العربية
Kutoa taarifa ya makubaliano ya utatuzi wa tatizo kwa Bodi
KIINGEREZA

Maelezo ya kina ya mradi

Namba ya mradiFP043
Kichwa cha habari cha mradi Mradi wa Kuhifadhi Maji wa Saïss
Mada
Kujibadili
Nchi Morocco
Mkoa
Afrika
Taasisi au shirika lililothibitishwa Benki ya Ulaya kwa ajili ya Ufufuzi na Maendeleo
Maeneo ya matokeo
Miundombinu na mazingira yaliyojengwa
Riziki za watu na jamii
Kundi la hatari Kundi B