Ripoti za ushauri
Muhtsari
Mfumo Huru wa Kupokea na Kurekebisha Malalamiko (IRM)· umepewa mamlaka ya kuripoti kwa Bodi juu ya masomo yaliyojifunza na ufahamu uliopatikana kutokana na kushughulikia kesi na kutoka katika mazoea mazuri ya kimataifa. Kulingana na masomo haya na ufahamu, Mfumo Huru wa Kupokea na Kurekebisha Malalamiko (IRM) unaweza kupendekeza upya sera, taratibu, miongozo na mifumo ya Mfuko wa Mabadiliko ya Tabianchi ya Kijani (GCF). Wakati ripoti ya ushauri inaandaliwa, Sekretarieti ya GCF· inaalikwa kutoa majibu ya usimamizi kabla ya ripoti kuchukuliwa na· Bodi ya GCF. Baada ya ripoti ya ushauri kuwasilishwa kwa Bodi, huchapishwa kwenye tovuti ya Mfumo Huru wa Kupokea na Kurekebisha Malalamiko (IRM).
Ripoti hii ya Ushauri juu ya kuzuia unyonyaji , matumizi mabaya na unyanyasaji kingono (P&PrSEAH) katika miradi na programu za Mfuko wa Mabadilko ya Tabianchi ya Kijani (GCF) unachota masomo muhimu kwa ajili GCF kutoka katika malalamiko mawili ambayo yaliwasilishwa kwa Jopo la Ukaguzi la Benki ya Dunia. Malalamiko hayo yalihusu matumizi mabaya na unyanyasaji wa kingono wa wanawake na wasichana kwa kivuli cha miradi miwili ya Benki ya Dunia nchini Uganda na DRC. Ripoti ya Ushauri inatoa mapendekezo ya jinsi gani GCF inaweza kuzuia na / au kupunguza hatari za unyonyaji , matumizi mabaya na unyanyasaji kingono (P&PrSEAH) kama sehemu ya ulinzi wake wa mazingira na kijamii. Ili kusoma Ripoti ya Ushauri na Majibu ya Usimamizi kutoka kwa Sekretarieti ya GCF, fuata viungo vilivyopo hapa chini:
- Ripoti ya Ushauri ya Mfumo Huru wa Kupokea na Kurekebisha Malalamiko (IRM) juu ya kuzuia unyonyajii, matumizi mabaya na unyanyasaji wa kingono katika miradi au programu za Mfuko wa Mabadiliko ya Tabianchi ya Kijani GCF
- Majibu ya Usimamizi ya Sekretarieti kwa Ripoti ya Ushauri ya Mfumo Huru wa Kupokea na Kurekebisha Malalalmiko (IRM)
- Uwasilishaji wa Video ya Ripoti ya Ushauri kwa Mfumo Huru wa Kupokea na Kurekebisha Malalalmiko (IRM) na Majibu ya Usimamizi wa Sekretarieti kwa Bodi B. 26
- Kuweka pamoja video za maoni yaliyotolewa na Bodi na Waangalizi Hai katika B.26